Open top menu
Alhamisi, 22 Agosti 2013


Mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney


KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho, amesema sakata la usajili wa mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney, ataliibua tena baada ya mchezo wao na miamba hiyo Jumapili katika Uwanja wa Old Trafford.

The Blues walishakataliwa ofa zao mbili kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji huyo asiye na furaha, huku kocha David Moyes akisisitiza kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa England hauzwi.

Lakini imegundulika kuwa United wanapanga kuanza tena mazungumzo na Chelsea kuona kama wanaweza kumchukua Juan Mata kama sehemu ya usajili wa mshambuliaji huyo, lakini Mourinho alisisitiza kuwa mazungumzo yataanza tena Jumatatu.

“Tulituma ofa (kwa ajili ya Rooney) na tutafanya hivyo tena," kocha huyo wa kireno alisema jana baada ya mchezo wa ushindi wa mabao 2-1 walioupata Chelsea dhidi ya Aston Villa.

"Lakini sitaki Chelsea ianze tena mazungumzo kabla ya kwenda kwao kwa ajili ya mchezo wetu wa ligi ... na hili ni kwa ajili ya miiko ya soka."

Jana usiku, Chelsea ilikuwa na kazi ngumu dhidi ya Villa, ambao walianza kwa bao la kujifunga wakati mchezaji wa Villa, Antonio Luna akiumalizia mpira wa Hazard, kabla ya Branislav Ivanovic kufunga bao la ushindi kwa kichwa na kuipa timu hiyo uongozi wa Ligi Kuu kwa muda.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments