Open top menu
Jumanne, 20 Agosti 2013




Mchezaji wa Yanga, Hamis Kiiza

Na Julius Kihampa
MSHAMBULIAJI wa kimataifa kutoka nchini Uganda anayechezea Klabu ya Yanga, Hamis Kiiza 'Diego', leo anatarajia kwenda nchini Lebanon kufanya majaribio ya wiki moja katika klabu ya Al Ahed inayoshiriki Ligi Kuu ya nchi hiyo.

Kiiza ambaye mpaka sasa ameshaitumikia Yanga kwa miaka miwili, aliongeza mkataba mpya wa miaka miwili na klabu hiyo kutokana na kumalizika kwa mkataba wake wa awali ambapo sasa mkataba wake utamalizika mwaka 2015.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa timu hiyo, Baraka Kizuguto alisema Al Ahed SC ni Mabingwa mara tatu wa Kombe la Ligi Kuu nchini humo, washindi mara nne wa Kombe la FA na washindi wa Kombe la Klabu Bingwa barani Asia mara sita ambapo wamekamilisha taratibu zote kwa ajili ya mchezaji kwenda kufanya majaribio.

Alisema Kiiza ataondoka leo jioni kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia ambapo atafanya mazoezi kwa siku saba kuanzia alhamisi na anatajiwa kurejea nchini mwisho wa mwezi huu.
Wakati huo huo, kikosi cha mabingwa hao, jana wameendelea na mazoezi katika viwanja vya shule ya Sekondari Loyola kujiandaa na mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ashanti United kwenye Uwanja wa Taifa jijini, Dar es Salaam.

Kizuguto alisema katika mchezo dhidi ya Azam wa kugombea Ngao ya Jamii wachezaji Kelvin Yondani, Mbuyu Twite na Ally Mustapha 'Barthez walipata majeraha kutokana na kuumizwa na John Bocco, Gaudence Mwaikimba na Kipre Tchetche hali zao zinaendelea vizuri.

"Leo (jana) wamefanya mazoezi mepesi isipokuwa Kelvin Yondani aliyepewa mapumziko na daktari kwa siku tatu kutokana na kupatiwa matibabu ya nyama ya paja aliyoumia siku ya mchezo huo na anatarajia kurejea uwanjani Jumatano kuungana na wachezaji wenzake katika mazoezi," alisema.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

Chapisho Jipya
This is the last post.

0 comments