Michuano ya Copa Coca-Cola kwa vijana wenye umri
chini ya miaka 15 inayoshirikisha mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani
inaanza kutimua vumbi Septemba 2 mwaka huu katika vituo sita tofauti.
Kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa leo (Agosti 29
mwaka huu), kituo cha Mwanza mechi zake zitachezwa katika viwanja vya Alliance
ambapo timu zitakazofungua dimba ni Kagera vs Kigoma, Mara vs Tabora, Simiyu vs
Geita na Mwanza vs Shinyanga.
Kituo cha Mbeya ambapo mechi zitachezwa viwanja vya
Iyunga ni Katavi vs Njombe, na Ruvuma vs Mbeya. Kituo cha Pwani ni Ilala vs
Kaskazini Unguja, na Lindi vs Pwani.
Ufunguzi katika kituo cha Arusha ambapo mechi zake
zitachezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid ni Manyara vs
Kilimanjaro, na Arusha vs Singida.
Uwanja wa Jamhuri ambapo utatumika kwa mechi za
kituo cha Morogoro, Tanga itacheza na Dodoma wakati Morogoro itaumana na
Temeke. Mjini Zanibar kwenye Uwanja wa Chuo cha Amaan ni kati ya Kaskazini
Pemba na Mjini Magharibi, na Kusini Pemba dhidi ya Kusini Unguja.
0 comments