Kocha wa klabu ya Bayern Munich Pep Guardiola
ameendeleza ubabe wake kwa Jose Mourinho anayeinoa Chelsea baada ya kutwaa
ubingwa wa Uefa Super Cup leo.
Guardiola ambaye alikuwa hasimu wa Mourinho alipokuwa
anaifundisha Barcelona huku Mreno huyo alipokuwa anaiongoza Real Madrid,
liibuka kidedea aliposhinda kwa mikwajua ya penalti 5-4.
Kiungo wa Bayern, Mario Goetze (kulia) akipambana
na Frank Lampard
Mchezo huo ambao ulikwenda kwa dakika 120 baada ya
90 kumalizika kwa sare ya mabao 1-1 na zilizpoongezwa dakika za nyongeza pia
miamba hiyo ilipata bao moja kila mmoja na kufanya mchezo huo umalize dakika
120 kwa sare ya mabao 2-2.
Mario Goetze (kushoto) akimiliki mpira mbele ya Frank
Lampard
Mabao ya Bayern yamefungwa na Franck Ribéry dakika
ya 47 na Javi Martínez dakika ya 120+1
wakati yale ya Chelsea yalifungwa na Fernando
Torres dakika ya 8′ na Eden Hazard dakika ya 93.
Manuel Neuer akishangilia ushindi sambamba na
mchezaji mwenzake, Frank Ribery
Waliofunga penalti kwa upande wa Bayern ni David
Alaba, Toni Kroos, Philipp Lahm, Franck Ribéry na Xherdan Shaqiri na mikwaju ya
Chelsea ilikwamishwa na David Luiz, Oscar, Frank Lampard na Ashley Cole,
aliyekosa ni Romeo Lukaku.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho akifuatilia
mchezo huo kwa staili ya kipekee.
Javi Martinez (kulia) akiifungia timu yake bao
la pili huku kipa wa Chelsea Petr Cech asijue la kufanya
Chini ya Ulinzi: Franck Ribery (katikati) akiwa
na mpira huku akizongwa na wachezaji wa Chelsea
0 comments