Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa TFF, Iman Omary Madega
Jumla ya wanamichezo 58 wamerudisha fomu kuomba
kuteuliwa
kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na ule wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL
Board) utakaofanyika Oktoba 27 mwaka huu.
Kwa upande wa TFF waliorejesha fomu kwa upande wa
urais ni Athuman Jumanne Nyamlani, Jamal Emil Malinzi, Omari Mussa Nkwarulo na Richard
Rukambura. Nafasi ya Makamu wa Rais wamejitokeza Imani Omari Madega, Nasib
Ramadhan na Walace Karia.
Walioomba nafasi za ujumbe kuwakilisha kanda
mbalimbali ni Abdallah Hussein Mussa, Kaliro Samson, Jumbe Odessa Magati,
Mugisha Mujwahuzi Galibona, Vedastus Kalwizira Lufano, Samwel Nyalla, Epaphra
Amana Swai, Mbasha Matutu Mong’ateko, Stanslaus Haroon Nyongo, Ally Mtumwa,
Elley Simon Mbise na Omari Walii.
Ahmed Msafiri Mgoyi, Yusuf Hamisi Kitumbo, Ayoub
Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja, Ayoub Shaib Nyenzi, Cyprian
Charles Kuyava, David Lugenge, Elias Mwanjala, Eliud Peter Mvela, John Mwachendang’ombe
Kiteve, James Patrick Mhagama, Kamwanga Rajabu Tambwe na Stanley William
Lugenge.
Athuman Kambi, Francis Kumba Ndulane, Zafarani
Damoder, Charles Komba, Hussein Mwamba, Stewart Ernest Masima, Farid Salum
Nahdi, Geoffrey Nyange, Riziki Majala, Twahil Twaha Njoki, Davis Elisa Mosha na
Khalid Abdallah Mohamed.
Wengine ni Alex Chrispine Kamuzelya, Juma Abbas
Pinto, Muhsin Balhabou, Omar Isack Abdulkadir, Shaffih Dauda Kajuna na Wilfred Mzigama
Kidao.
Kwa upande wa uchaguzi wa TFF mwombaji ambaye
hakurudisha fomu ni Venance Mwamoto pekee. Kwa upande wa TPL Board
waliojitokeza kuwania uongozi wa juu ni wawili tu; Hamad Yahya Juma
(Mwenyekiti) na Said Muhamad Said (Makamu Mwenyekiti).
Walioomba nafasi za ujumbe wa TPL Board ni Kazimoto
Miraji Muzo, Michael Njunwensi Kaijage, Omari Khatibu Mwindadi, Salum Seif
Rupia na Silas Masui Magunguma.
0 comments