MREMBO
wa Tanzania, Brigitte Alfred ameonyesha mfano wa kuigwa nchini katika tasnia
hiyo baada ya kuanza ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi
(albino) katika wilaya ya Shinyanga wanaoishi katika shule maalum ya Buhangija.
Tayari
mrembo ameweka jiwe la msingi na kupandisha ukuta sambamba na kukabidhi mabati
200 kwa ajili ya kujengea paa la bweni hilo la wavulana lenye uwezo wa kulaza
wanafunzi 50.
Makabidhiano
hayo yalifanywa na mrembo huyo kwa katika hafla fupi iliyohudhuriwa na mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi, afisa elimu wa manispaa ya Shinyanga
Honoratha Ruhumbika na walimu wa shule hiyo wakiongozwa na mwalimu mkuu, Peter
Ajali.
Briggite
alisema kuwa ameamua kutimiza ahadi yake aliyoitoa mwezi Aprili mwaka huu
alipotembelea Shinyanga kwa kazi za jamii na kuona changamoto za watoto
wanaosoma katika shule hiyo.
Alisema
kuwa mpango huo upo katika mpango wa Miss Tanzania ujulikano kwa jina la Urembo
wenye malengo maalum (Beauty with Purpose) nay eye kuamua kufanya kwa vitendo.
“Ni
faraja kwangu kuona kuwa ninatimiza ahadi yangu, nawashukuru wote walionisaidia
ikiwa pamoja na familia yangu, na ninaomba wengine wanisaidie kwani badi kuna
changamoto nyingi katika ujenzi na kazi za jamii kwa ujumla,” alisema Brigitte.
Alisema
kuwa amepania kuweka historia katika fani hiyo kwani anaamini ujenzi au jingo
hilo litakuwa kumbukumbu kubwa kwake tena kwa vizazi na vizazi.
Brigitte
pia aliwataka wanafunzi hao kutokata tamaa hata kwa wale wasiokuwa karibu na
familia zao na kwamba wamtegemee zaidi Mwenyezi Mungu kwa kuwa yeye ndiye
mfariji kwa wanyonge huku akiwahimiza kuzingatia zaidi elimu kwani ndiyo msingi
wa maisha yao.
“Nilipata
msukumo wa kuisaidia shule hii hususani katika ujenzi wa bweni hilo kutokana na
ujio wake wa mwezi Aprili mwaka huu shuleni hapo na kujionea adha wanayopata
watoto hao kutokana na msongamano mkubwa mabwenini,” alisema.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi alimpongeza Brigitte kwa moyo huo wa
kujitolea na kuwataka warembo wengine kuiga mfano wake.
Nyamubi
alisema kuwa alichokifanya Brigitte ni jambo la kukumbukwa nan i msaada mkubwa
kwa jamii hasa kwa watu wenye ulemabu wa ngozi.
Mkuu
huyo wa wilaya aliwaomba wazazi wa watoto hao kuwa na tabia ya kuwatembelea
watoto wao mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kuwachuku wakati wa likizo.
Naye
mwalimu mkuu wa shule hiyo Peter Ajali alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo la msongamano mabwenini kwani kuna jumla ya
watoto 247 huku mabweni yaliyopo yana uwezo wa kukaa watoto 148 tu.
0 comments