Open top menu
Jumatano, 21 Agosti 2013



Klabu ya Yanga imewatoa hofu waliokuwa wachezaji wao Shadrack Nsajigwa, ambaye kwa sasa ni kocha wa Lipuli ya Iringa na Stephano Mwasika aliyesajiliwa Ruvu Shooting kwamba watawalipa fedha zao wanazowadai.

Mwalusako alisema wamepata taarifa zisizo rasmi kwamba  wachezaji hao wamewasilisha malalamiko yao kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakida hawataki kuwalipa, jambo ambalo si kweli.

"Tunafanya mawasiliano ya mara kwa mara na wachezaji hao na mwingine anadai yupo mbali, hivyo mchakato wa kuwalipa fedha zao upo kama kawaida ila kwa sasa tunaweka mambo sawa na tutawalipa siku si nyingi," alisema.
Nsajigwa anaidai klabu yake hiyo ya zamani Sh. 10 milioni, huku Mwasika naye akidai milioni sita.

Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments