Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na
kampuni ya Azam Media leo (Agosti 30 mwaka huu) wamesaini mkataba wa haki za
kipekee za televisheni (exclusive rights) utakaoiwezesha Azam TV kuonesha mechi
za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
Mkataba huo wa miaka mitatu wenye thamani y ash.
5,560,800,000 umesainiwa kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Makamu
wa Rais, Athuman Nyamlani amesaini kwa niaba ya TFF wakati aliyesaini kwa
upande wa Azam Media ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Thys Torrington.
Ligi Kuu ya Tanzania sasa itakuwa ikipatikana
kupitia kisimbuzi (decorder) cha Azam TV kitakachokuwa na chaneli zaidi ya 50.
Mechi hizo zinatarajiwa kuoneshwa moja kwa moja wakati wowote kuanzia mwezi
ujao.
Makamu wa Rais wa TFF, Nyamlani amesema udhamini huo
wa televisheni ni fursa pana kwa klabu kwani zitaweza kujitangaza zaidi huku
wachezaji nao wakipata soko zaidi za mpira wa miguu.
0 comments