Open top menu
Jumapili, 25 Agosti 2013


MSHAMBULIAJI wa zamani wa klabu ya Manchester United, Cristiano Ronaldo amewaambia viongozi wa timu hiyo, kuwa mipango yake ni kuona siku moja anaichezea tena klabu hiyo.

Ronaldo ambaye aliuzwa na Manchester mwaka 2009 kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi ya pauni 80 milioni kwa Real Madrid, amekuwa akihusishwa na kutaka kuihama klabu hiyo na kurudi tena Old Trafford.

Leo mshambuliaji huyo raia wa Ureno amevunja ukimya baada ya kuwaambia Manchester United kuwa lazima atarudi kuichezea tena timu hiyo na hata kama haitakuwa katika kipindi hiki cha usajili basi itakuwa mwakani katika kipindi cha usajili cha majira ya joto.

Ronaldo ambaye mkataba wake na klabu ya Madrid unatarajiwa kumalizika 2015 lakini ni ngumu kumaliza mkataba wake kwani kuna dalili nyingi kuwa staa huyo amechoka maisha ya Bernabeu.

Manchester United ambao hawajazungumza kitu katika mipango hiyo lakini wanaonekana wanajiandaa kumpokea mshambuliaji huyo kwani tayari jezi namba saba ambayo msimu uliopita alikuwa akivaliwa na Antonio Valencia amepokonywa na kuachwa ikiwa haina mtu.

Ronaldo alipokuwa Manchester United alikuwa akivaa jezi namba saba hivyo wameshamuandalia mazingira ya kumrudishia jezi yake pindi atakaporejea Old Trafford.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments