Open top menu
Jumatano, 21 Agosti 2013





IKIWA yamebaki masaa 48 kabla ya kufungwa kwa dirisha na usajili wa Ligi Kuu ya England, klabu ya Manchester United imekubali kuzungumza na Chelsea ili kumwachia mshambuliaji wao, Wayne Rooney kwa kubadilishana na Juan Mata.

Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho aliekeza nguvu zake kwa Rooney baada ya kuwakosa washambuliaji aliokuwa anawawinda, Radamel Falcao, Edinson Cavani na Robert Lewandowski lakini Kocha wake, David Moyes alisisitiza kuwa nyota huyo yupo kwenye mipango yake na hawezi kuuzwa.

Baada ya kuwa na presha kubwa kutoka kwa Chelsea inaonekana Man Utd wamelegeza kamba na kufungua milango ya mashambuliaji huyo wa England kuondoka katika Uwanja wa Olkd Trafford.

United ambao walipanga kumwachia Rooney kwa pauni milioni 40 (zaidi ya Sh 88 bilioni) lakini Chelsea walifika dau ya pauni 30 milioni (Sh 66 bilioni), hivyo sasa mpango huo unaweza kukamilika kama wakimtoa fedha hizo pamoja na Mata.

Pande hizo mbili kwa pamoja zipo katika makubaliano ya kubadilishana wachezaji hao lakini Chelsea kuna uwezekano wa kumuongeza na David Luiz katika mpango huo ili iweze kuwashawishi United kumwachia Rooney kwa urahisi zaidi.

"Wayne (Rooney) anaigiza kwa kufanya mazoezi bila kinyongo na wenzake katika uwanja wa Carrington lakini hakuna siri kuwa mipango yake ni kuondoka," alisema chanzo cha habari kutoka ndani ya Man United.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments