Open top menu
Jumanne, 20 Agosti 2013


Phil Bardsley

BEKI wa timu ya soka ya Sunderland,
Phil Bardsley, amesimamishwa kufanya mazoezi na timu hiyo na kocha wake, Paolo Di Canio, baada ya kutoa lugha ya kuikebehi timu hiyo kwa kipigo walichopata dhidi ya Fulham.

Mtandao wa Sportsmail asubuhi ya leo ulikuwa wa kwanza kuandika kuwa Bardsley anaweza kuwa matatizoni kutokana na maoni yake juu ya mwanzo mbaya wa timu yao kwa kuchapwa 1-0 nyumbani juzi JUmapili.

Na kocha huyo mkali wa Sunderland alikuja juu ghafla na kumwambia Bardsley asionekane katika Uwanja wa mazoezi wa Academy of Light. Na haijajulikana kama beki huyo atakuwa katika kifungo hicho kwa muda gani.

Bardsley alituma ujumbe kwa mashabiki wa klabu hiyo katika mtandao wa Instagram na kutuma picha yake huku akiandika writing: 'Mwanzo mzuri. Hahahhahaha hahahhaha!!!’

Na hilo lilizua hasira kwa mashabiki wa klabu hiyo ambao walichukizwa na mwanzo mbaya wa timu yao na Bardsley alitakiwa kutoa maelezo mbele ya kocha na viongozi wengine wa klabu hiyo kutokana na matamshi yake.
Sportsmail liliandika kuwa beki huyo wa zamani wa Manchester United angeweza kutimuliwa kwa 'hasira'.
Na sasa inasemekana kuwa mchezaji huyo anaweza kuuzwa haraka ndani ya siku chache zijazo, huku uongozi ukionekana kushindwa kumtetea kutoka katika hasira ya Di Canio.
Hii ni mara ya pili kwa Bardsley kuitia hasira klabu hiyo, Di Canio na kwa kwa mashabiki kupitia mtandao.

Mei mwaka huu, kabla ya mchezo wao wa mwisho wa ligi dhidi ya Tottenham Hotspur, alionekana katika picha akiwa katika klabu ya usiku ya Newcastle akizungukwa na fedha kiasi cha pauni 50. Aliondolewa katika kikosi cha mchezo huo na kutumia muda wote wa majira ya joto akifanya mazoezi na kikosi B (chini ya miaka 21) kabla ya kuumia wiki iliyopita katika mchezo wa kirafiki.
Bardsley hakupewa namba na Di Canio wiki iliyopita. Nahodha Lee Cattermole, ambaye hakuwahi kucheza chini ya kocha Di Canio, alikuwa pia akinyimwa hata namba ya jezi hadi alipopewa 33 katika orodha ya wachezaji wapya.

Na badala yake, namba aliyokuwa akitumia, yaani namba 6 alipewa mchezaji mpya aliyesajiliwa hivi karibuni, Cabral, mmoja kati ya wachezaji watano wapya ambao watacheza katika mchezo wao ujao.
Kocha wa Sunderland, Pablo Di Canio
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments