Open top menu
Ijumaa, 13 Septemba 2013


WASANII wa Hip Hop Tanzania na nje ya Tanzania wanatarajiwa kupanda jukwaa moja katika tamasha la Tanzania Hip Hop Music Festival litakalofanyika kwenye Ukumbi wa New Msasani Club.

Tamasha hilo ambalo lililoandaliwa na Kundi la Kikosi cha Mizinga linatarajiwa kufanyika Septemba 20 mwaka huu likiwa na lengo la kuwakutanisha wasanii wa muziki huo wa Hip Hop wa ndani na nje ya nchi.

Akizungumza na Nyumba ya Michezo na Burudani, kiongozi wa kundi hilo, Kalapina alisema tamasha hilo litakutanisha wasanii kutoka katika nchi mbalimbali kwa lengo la kubadiliashana ujuzi ikiwa na pamoja na kufikisha ujumbe wao kwa jamii kwa ujumla.

Kalapina aliwataja wasanii ambao watakaotumbuiza ni pamoja na Cashmere kutoka New York, Marekani, Kimya wa Kenya wakati wasanii wa nyumbani watakaopanda jukwaani ni LWP, Manzese Crew, Mchizi Mox, Big Dog PoseSerious Manizzle, Viraka, Montel Foster na Kikosi cha Mizinga.

Kiongozi huyo alisema mbali na wasanii hao kushambulia jukwaa lakini pia kutakuwa na mashindani ya freestyle pamoja na kucheza brake dance, kiingilio katika tamasha hilo kitakuwa sh. 50,000 na milango itakuwa wazi kuanzia saa 10 jioni.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments