Open top menu
Jumamosi, 14 Septemba 2013

KLABU ya Simba leo imefanikiwa kuongeza pointi tatu baada ya kuitandika timu ya Mtibwa Sugar mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa dakika zote tisini lakini bahati ilikuwa kwa Simba ambao walifanikiwa kupata bao la kwanza dakika ya 69 lililofungwa kwa kiungo wake, Henry
Joseph.

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Haruna Chanongo akiruka kwanja la beki wa Mtibwa, Hassan Ramadhani.

Wakati mashabiki wa Simba wakiamini kuwa wameshinda bao 1-0 katika mchezo huo mshambuliaji wake, Betrum Mombeki dakika za nyongeza aliifungia Simba bao la pili na kuwafanya Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

 Kiungo wa Simba, Ramadhani Singano 'Messi' akimtoka mchezaji wa Mtibwa Sugar
 Mfungaji wa bao la kwanza la Simba, Henry Joseph 'Shindika' akitambaa na mpira katika mchezo huo
 Beki wa Simba, Issa Rashid 'Baba Ubaya' akimtoka beki wa Mtibwa, Hassan Ramadhani

Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments