Open top menu
Jumatatu, 16 Septemba 2013


 STAA wa Uholanzi, Robin van Persie ametuliza mizuka na mashabiki na wapenzi wa klabu yake ya Manchester United baada ya kuweka wazi kuwa ana mpango wa kuitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal amesema kuwa malengo yake ni kucheza kwa kiwango cha juu na kuisaidia timu yake kutwaa mataji mengi zaidi.

Mdachi huyo ambaye kwa sasa bado ana mkataba wa miaka mitatu amefunguka na kusema kuwa anapenda kuongeza mkataba mwingine zaidi akiwa Manchester United.

Nyota huyo mwenye miaka 30 sasa alijiunga na mwanzoni mwa msimu uliopita na kufanikiwa kutwaa taji alke la kwanza la Ligi Kuu ya England msimu uliopita akiwa na Manchester United na amekuwa na matumaini makubwa ya kuendelea kuvaa medali za dhahabu akiwa na klabu hiyo.

"Nina mkataba wa miaka mitatu na napenda kuendelea kuwa hapa kwa muda mrefu zaidi," alisema Van Persie alipokuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha klabu hiyo.

"Nataka kucheza hapa kwa kadri itakavyowezekana tena kwa kiwango cha hali ya juu. Kushinda mataji mengi zaidi ndiyo lengo langu kwa sasa."
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments