Open top menu
Jumamosi, 14 Septemba 2013

Kiungo wa Arsenal, Jack Wilshare



KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kiungo wake,Jack Wilshere atang'ara katika fainali za Kombe la Dunia zitakazopigwa nchini Brazil, mwakani.

Kiungo huyo, 22 hakuonesha kiwango kizuri kwa taifa lake wakati wa mechi yao dhidi ya Ukraine Jumanne iliyopita iliyomalizika kwa kutoka suluhu.

Lakini Wenger alimtetea kiungo wake matokeo ya mechi hiyo na kwamba ana uwezo na tabia zinazofanana na kiungo wa Ufaransa, Zinedine Zidane kuwa kiungo tegemezi kwa taifa hilo.

"Kama Jack Wilshere atacheza kama anavyocheza akiwa Arsenal tunaweza kusema poa, leo hakuwa katika kiwango chake, lakini anavyocheza hivyo katika timu ya taifa kila mmoja ana hoji uwezo wake," alisema Wenger.

"Timu ya taifa siku zote huhitaji watu ambao wanaweza kuhimili presha hizo, sisi (Wafaransa) tulikuwa naye Zidane ambapo Ufaransa ikicheza vizuri ujue ni Zidane  huyo lakini wengine wanaweza lakini si kama Zidane.Tunahitaji vizazi vipya lakini pia kuwa na aina ya kipekee ya mchezaji."

"Tuwe wakweli.Jack anaweza kufanya hiyo kazi.Ni kijana,22, ana uwezo wa kufanya hivyo lakini anahitaji kucheza miezi sita bila ya kuwa na majeruhi au tatizo lolote."

"Jack ana kila sababu ya kuwa juu, mchezaji wa juu.Amepitia mazingira

magumu," kocha huyo aliongeza.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments