Open top menu
Jumanne, 24 Septemba 2013


TIMU ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake ‘Twiga Stars’ imepangiwa kucheza na Zambia katika mechi za kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika mwakani nchini Namibia.

Twiga Stars itaanzia ugenini jijini Lusaka ambapo mechi ya kwanza itachezwa kati ya Februari 13 na 15 mwakani wakati ile ya marudiano itafanyika kati ya Februari 28 na Machi 2 mwakani jijini Dar es Salaam.

Iwapo Twiga Stars itafanikiwa kuitoa Zambia, raundi ya pili ambayo ndiyo ya mwisho itacheza na mshindi kati ya Botswana na Zimbabwe. Mechi ya kwanza itakuwa Dar es Salaam kati ya Mei 23 na 25 mwakani wakati ile ya marudiano itakuwa kati ya Juni 6 na 8 mwakani.

Nchi 25 zimeingia katika mashindano huku mabingwa watetezi Equatorial Guinea, makamu bingwa Afrika Kusini na Cameroon iliyoshika nafasi ya tatu katika fainali zilizopita zikiingia moja kwa moja katika raundi ya pili.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments