Open top menu
Jumatano, 25 Septemba 2013




























KOCHA Brendan Rodgers ameliambia gazeti la Guardian la England kuwa hahofii kumtumia Luis Suarez katika kikosi cha Liverpool kinachokipiga na Manchester United leo katika mchezo wa kwanza wa Capital One Cup.

Suarez yuko katika listi ya Rodgers tena baada ya kufungiwa michezo 10, huku akiukosa mchezo wa kichapo cha bao 1-0 walichokipta mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Southampton, kifungo alichokipata baada ya kumng'ata kwa makusudi beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic, msimu uliopita.

Na anatarajiwa kurudi katika mchezo huo unaopigwa leo kwenye Uwanja wa Old Trafford, wakati mchezaji huyo pia akikumbukwa kwa kufungiwa michezo nane kwa kumtolea lugha ya kibaguzi beki wa United, Patrice Evra 2011.

Rodgers anaamini kuwa Suarez atakuwa tayari kupokea mapokezi mabaya Old Trafford. Na alisema: "Sihofii chochote juu ya kumpanga Luis. Tangu nimekuwa hapa sikuwahi kukutana na kitu kama hicho. Kuna historia katika michezo hii lakini sielekezi akili yangu huko.

"Luis ni mchezaji mwenye jina kubwa. Na ni mmoja kati ya wachezaji wakubwa wenye matukio ambaye nimewahi kukutana naye katika maisha yangu. Sidhani kama mapokezi yatamchanganya.

"Ni mpiganaji na malengo yake ya kufanikiwa yapo kwa ajili ya kila mmoja kumuona. Tunafurahikuona kuwa amerudi kikosini. Najua hata wachezaji wana furaha kurudi kwa mchezaji huyu uwanjani kutokana na ubora wake."

Rodgers aliongeza: "Sidhani kama atakuwa katika ulinzi mkubwa kama ambavyo imekuwa katika michezo iliyopita. Luis ni aina hiyo ya mchezaji. Siku zote huzungumza anapochezewa vibaya. Kazi anayofanya anapokuwa ndani na karibu na eneo la hatari huwafanya mabeki kuwa katika wakati mgumu.

"Ni sehemu ya mchezo na unatakiwa kuendana nayo. Nafikiri huu ni mchezo mzuri kwetu baada ya kutoka vichwa chgini katika mchezo uliopita dhidi ya Southampton. Luis atakuwa sehemu ya mchezo huu.

"Nina uhakika kuwa wakati Luis atakapojua kuwa ni sehemu ya mchezo huu, itamshitua na kumfanya kuwa tayari kwa kutetea timu yake. Unaweza kuona kwamba huu ni mchezo mzuri kwake kwa ajili ya ujio mpya baada ya adhabu."
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments