Open top menu
Jumatano, 18 Septemba 2013


 BAADA ya kuongeza mkataba wa kuitumikia klabu ya Madrid na kuwa mchezaji anayelipwa ghari kuliko wote katika Ligi Kuu ya Hispania, mshambuliaji Cristiano Ronaldo ameonyesha thamani yake kwa klabu hiyo.

Jana usiku Ronaldo aliiongoza timu yake kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya Galatasaray ya Uturuki katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa kwenye Uwanja wa Turk Telekom Arena.

Katika mchezo huo Ronaldo ameongeza rekodi nyingine baada ya kufunga hat-trick katika mchezo huo na kuwa pekee wa Real Madrid aliyefunga mabao matatu katika mchezo mmoja ndani ya michuano hiyo.

Kwa mabao hayo Ronaldo pia ameshika nafasi ya nne kwa wachezaji waliofunga mabao mengi katika michuano hiyo baada ya kufikia mabao 53, akiwa nyuma ya Ruud van Nistelrooy aliyefunga mabao 56, Lionel Messi mabao 59 wakati kinara ni Raul aliyefunga mabao 71.

Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments