Open top menu
Jumapili, 15 Septemba 2013


NDOTO za mashabiki wa Manchester United za kumuona mshambuliaji wao wa zamani, Crstiano Ronaldo akivaa tena jezi zao zimeyeyuka leo asubuhi baada ya nyota huo kuongeza mkataba wa miaka mitano ya kuitumikia klabu yake ya Real Madrid.

Ronaldo ambaye mkataba wake wa awali ulikuwa ufikie ukingoni mwaka 2015, mara kadhaa amekuwa akihusishwa na kurudi katika klabu yake ya zamani ya Manchester United.

Nyota huyo wa Uren oleo asubuhi amesaini mkataba mpya wenye thamani ya pauni 75 milioni (zaidi ya Sh 165 bilioni) lakini pia mtakaba huo amekuwa ndiye mchezaji anayelipwa zaidi nchini Hispania.

Tovuti ya klabu hiyo yenye maskani yake Santiago Bernabeu imethibitisha kuingia mkataba na nyota huyo baada ya kukubaliana na mahitaji yake ambayo sasa atakuwa analipwa zaidi kuliko wachezaji wote nchini humo.

Los Blancos hawajatoa wazi makubaliano yaliyomo kwenye mkataba huo lakini wamethibitisha nyota huyo kuwa atalipwa zaidi kwani katika miaka mitano ya mkataba wake atalipwa pauni 17 milioni (zaidi ya Sh 42.5 bilioni) kutokana na mshahara kamili atakaokuwa analipwa na klabu hiyo.

Kutokana na makubaliano hayo Ronaldo amewaacha mbali wachezaji nyota kama Lionel Messi wa Barcelona na Gareth Bale aliyesajiliwa hivi karibuni kwa usajili uliovunja rekodi ya dunia.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments