Open top menu
Ijumaa, 6 Septemba 2013


BEKI wa kati wa Chelsea, David Luiz, amesema ameamua kubaki katika klabu yake ya sasa kwa kukataa ofa ya Barcelona licha ya kutangaziwa dau nono.
Beki huyowa kimataifa wa Brazil alikuwa katika rada za Barca kutokana na timu hiyo kutaka kuimarisha safu yao ya ulinzi, lakini alisisitiza kuwa ana majukumu ya kuifanyia miamba hiyo ya Stamford Bridge chini ya Jose Mourinho.

Akizngumza na gazeti la michezo la Brazil, Gazeta Esportiva, Luiz alisema: "Kulikuwa na ofa maalumu [kutoka Barcelona], lakini niliamua kwa makusudi kubaki Chelsea.

"Nina furaha kucheza katika klabu kubwa  na kuwa katika kikosi cha timu ya taifa kwa ajili ya kuliwakilisha taifa langu."

Barcelona ilidaiwa kutangaza dau la pauni milioni 21.5 kwa ajili ya kumsajili Luiz Agosti mwaka huu, kiasi ambacho kilikuwa ni kidogo kwa Chelsea kushawishika kumuachia mchezaji huyo mwenye miaka 26.

Barca walikuwa wakimtaka Luiz kama mbadala wa beki wa Paris Saint-Germain, Thiago Silva, ama beki wa Liverpool, Daniel Agger, lakini walishindwa kuwasajili wote.


Majaaliwa ya kurudi uwanjani kwa Nahodha wa Barca, Carles Puyol yamekuwa shakani na kuamua kutaka kusajili mchezaji mwingine, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Michezo wa Barca, Andoni Zubizaretta.








Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments