Open top menu
Jumatatu, 2 Septemba 2013


Kiungo Mshambuliaji wa Real Madrid, Mesut Ozil ametua rasmi katika klabu ya Arsenal kwa mkataba wa miaka mitano, lakini mshambuliaji wa Chelsea, Demba Ba bado kidogo kumalizana na klabu hiyo ya Emirates.

Ozil amemwaga wino kuitumikia Arsenal kwa misimu ijayo baada ya kocha Arsene Wenger kukubali kulipa pauni 47 milioni (zaidi Sh 103 bilioni).

Wenger ambaye amekuwa akilaumiwa kwa ubairi, amevunja benki kwa kuvunja rekodi ya timu hiyo kwa kumsajili mshambuliaji huyo wa Ujerumani ambaye atakuwa analipwa pauni 150,000 kwa wiki.
Arsenal nayo ipo mbioni kumnasa Ba ambaye amekosa namba katika kikosi cha Jose Mourinho anatarajia kumalizana na klabu hiyo wakati wowote kuanzia sasa kwani mazungumzo ya awali yanakwenda vizuri.

Katika mazungumzo ya awali Arsenal imekubaliana na Chelsea kuuziwa mchezaji huyo kwa mkopo kwa ada ya uhamisho wa pauni 2 milioni kwa mwaka mmoja.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments