Open top menu
Ijumaa, 13 Septemba 2013


YANGA imepewa siku 14 kuanzia leo (Septemba 13 mwaka huu) kuwalipa waliokuwa wachezaji wake msimu uliopita, nahodha Shadrack Nsajigwa na Stephen Mwasika wanaoidai klabu hiyo jumla ya sh. milioni 15.5.

Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana (Septemba 12 mwaka huu) ambapo pamoja na mambo mengine ilisikiliza madai ya wachezaji hao.

Fedha hizo ni ada ya usajili ambayo klabu hiyo ilikubaliana na wachezaji hao wakati ikiwasainisha mikataba. Yanga imeshawalipa sehemu ya fedha walizokubaliana na kiasi hicho ndicho bado hakijalipwa. Nsajigwa anadai sh. milioni 9 wakati Mwasika ni sh. milioni 6.5.

Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments