Open top menu
Ijumaa, 20 Septemba 2013


MSHAMBULIAJI wa klabu ya Yanga, Mganda Hamis Kiiza amerejea kundini juzi usiku na leo amejiunga na mazoezini na uwezekano akaanza kwenye mchezo wa timu hiyo dhidi ya Azam Jumapili.

Kiiza ambaye hajaitumikia klabu hiyo tangu kuanza kwa msimu huu baada ya kuwa nchini Lebanon kwa ajili ya majaribio ya wiki mbili lakini nyota huyo aliporudi aliunganisha kwao Uganda na huko alijiunga na timu yao ya Taifa.

Mshambuliaji huyo amejiunga na wachezaji wenzake katika mazoezi ya leo asubuhi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola na anaweza kutumiwa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Azam Jumapili.

Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi Ernie Brandts ameiambia Nyumba ya Michezo na Burudani, alisema atamuangalia nyota huyo katika mazoezi ya kesho asubuhi kabla ya kuamua kumtumia katika mchezo wa Jumapili dhidi ya Azam.

Brandts alisema mazoezi ya kesho ndiyo yatatoa kikosi cha Jumapili na siyo kwa kumuangalia Kiiza peke yake. Akiona kama mshambuliaji huyo yupo fiti kwa mchezo huo atamtumia lakini aliporidhishwa naye ataanzia benchi.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments