Open top menu
Jumatatu, 16 Septemba 2013


BAADA ya mashabiki na uongozi wa klabu ya Manchester United kuchomwa na mkuki wa moyo kutokana na taarifa za mshambuliaji wao wa zamani Cristiano Ronaldo kusaini mkataba mpya wa Real Madrid, nyota huyo amewatonesha jearaha hilo.

Staa huyo wa Ureno aliyekuwa akihusishwa na madai ya kurudi katika klabu yake ya zamani, jana asubuhi aliongeza mkataba wa miaka mitatu utakaofikia kikomo 2018 wa kuichezea Madrid na kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika Ligi Kuu ya Hispania.

Ronaldo hadi sasa ameshaifungia timu yake ya Madrid mabao 203 tangu alipotua klabuni hapo, amesema hana mpango wa kurudi tena katika klabu yake ya zamani kwani ile itabaki kuwa historia tu, sasa yeye ni mchezaji wa Madrid.

"Niwe mkweli kwako. Kila mtu anajua kuwa nilikuwa Manchester kwa miaka sita, na walinipa vitu vingi na siwezi kusahau hilo," alisema Ronaldo.

"Lakini Manchester imepita, sasa ni Madrid. Hana ni nyumbani kwangu, familia yangu ipo hapa. Nina furaha sana kuwa hapa.

"Ninaiheshimu klabu yoyote ambayo inagonga hodi na kuniulizia kuhusu mimi, lakini wanatakiwa kujua kuwa mipango yangu kwa sasa ni kubaki hapa na kuichezea klabu hii labda hadi mwisho wa maisha yangu ya soka.”
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments