Open top menu
Jumatatu, 16 Septemba 2013


SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) wametoa ratiba ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia kwa timu za Afrika mwaka ambapo raundi ya kwanza itachezwa Oktoba wakati mchezo wa marudiano itachezwa mwezi Novemba mwaka huu.

Ratiba hiyo ambayo imejumuisha timu zilizofuzu hatua ya makundi ambazo ni Ivory Coast, Ethiopia, Ghana, Nigeria, Misri, Senegal, Tunisia, Cameroon, Burkina Faso na Algeria.

Kwa mujibu wa hatua hiyo raundi ya kwanza itachezwa kati ya Oktoba 11 na 13 wakati miamba hiyo itarudiana kati ya Novemba 15 na 19 mwaka huu, michezo ambayo itakuwa imetoa wawakilishi wanne watakaoiwakilisha Afrika katika fainali hizo zitakazofanyika nchini Brazil.
Ratiba hiyo iliyotolewa na Caf muda mchache uliopita inaonyesha kuwa wawakilishi pekee wa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Ethiopia watavaana na Nigeria, Misri watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Ghana.

Ivory Coast wamepangiwa na Senegal, Tunisia watapepetana na Cameroon wakati Burkina Faso wanawania tiketi ya kucheza fainali hizo dhidi ya Algeria.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments