Open top menu
Alhamisi, 26 Septemba 2013


BAADA ya kupata matatizo nchini Afrika Kusini, msanii wa kizazi kipya, Mgaza Pembe anayefahamika zaidi kama M 2 THE P, ameamua kwenda nyumbani kwao Mlandizi kusaka ubani kwa kufanya onyesho kwa wakazi wa mji huo.

M 2 THE P ambaye alikutwa na matatizo na msanii mwenzake, Albert Mangwea ambaye alifariki dunia, amefyatua kibao chake kipya alichokipa jina Masambe Wena (Twenzetu sasa) ambacho kimekuwa kinafanya vizuri katika radio na televisheni za hapa nchini.

Msanii huyo aliiambia Nyumba ya Michezo na Burudani kuwa ameamua kufanya onyesho hilo maalum kwa ndugu zake wa Mlandizi katika Ukumbi wa Super Night ikiwa sehemu ya shukrani kwa kumuomba wakati wa matatizo.

“Toka nimerudi na kufanya kazi yangu ya muziki nilikuwa sijawahi kuja nyumbani kufanya onyesho lolote,” alisema M 2 THE P. “Show hii ni maalumu kwa watu wangu wa Mlandizi kwa lengo la kuwapa shukrani kwa maombi yao.

“Nimefanya show nyingi nje ya kwetu katika Fiesta, nikaona kuna sababu ya kurudi nyumbani kushow love na ndugu zangu.”

Alisema kiingilio katika show hiyo kitakuwa Sh 3,000 kwa lengo la kumfanya kila mtu awe na uwezo wa kuingia na kupata burudani kutoka kwa msanii wao na wale watakaomsindikiza.

Wasanii ambao watamsindikiza M 2 THE P katika show hiyo ni Country Boy, Nyandu Tozi, Mirrow, Luteni Kalama, Isabela wa Scorpion Girls, Suma G, Shantiwa, Kionee, Ally Maowa na Punchiz Niggaz.


Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments