Open top menu
Jumatatu, 23 Septemba 2013


Naibu Waziri wa Utamaduni Vijana na Michezo, Amos Makala (wa tatu kulia) akimkabidhi kikombe Nahodha wa Topland ya Kinondoni, Dar es Salaam, Omari Akida mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za kitaifa za mashindano ya Safari Pool 2013 yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani Morogoro

KLABU ya Top Land kutoka mkoa wa kimichezo wa Kinondoni jijini Dar es Salaam wameibuka mabingwa katika fainali za kitaifa za mashindano ya Safari Pool 2013, yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani Morogoro.

Top land walitwaa ubingwa huo kwa kuifunga klabu ya Mpo Afrika ya Temeke 13-10 na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 5,000,000,  Kikombe na medali za dhahabu kwa kila mchezaji.

Mshindi wa pili katika fainali hizo ni klabu ya  Mpo Afrika ambayo ilizawadiwa Sh. 2,500,000 na medali za fedha kwa kila mchezaji wakati mshindi wa tatu  ni klabu ya Supersport kutoka mkoa wa Manyala ambao walizawadiwa Sh. 1,250,000 na medali za shaba na mshindi wa nne ni klabu ya Mashujaa wa Ilala ambao walipata Sh. 1,000,000.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume (single), mchezaji Festo Yohana kutoka klabu ya Mashujaa alitwaa ubingwa wa Taifa kwa kumfunga Mussa Mkwega kutoka Morogoro 5-1 na kuzawadiwa Sh.700,000, kikombe na medali ya dhahabu ambapo mshindi wa pili alikuwa Mussa Mkwega aliyepata Sh. 350,000 na medali  ya Fedha.

Mshindi wa tatu ni Mohamed Idd wa Atlantic ya Dodoma ambaye alijizolea Sh 200,000 na medali ya shaba ambapo mshindi wa nne ni Ernest John kutoka Tabora ambaye alizawadiwa Sh. 150,000.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanawake (Singles), mchezaji Rose Deus kutoka Morogoro alitwaa ubingwa wa kitaifa kwa kumfunga Cecilia Kileo kutoka Ilala 5-4 na hivyo Rose kuzawadiwa Sh 350,000 na kikombe na medali ya Dhahabu ambapo Cecilia alikamata nafasi ya pili na kupata Sh 200,000 na medali ya Fedha.

Nafasi ya tatu ilichukuliwa na mchezaji Merry Gumbu kutoka Arusha ambaye alizawadiwa Sh 150,000 na medali ya shaba wakati Judith Machafuko alishika nafasi ya nne na kuweka kibindoni Sh 100,000.

Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

Maoni 1 :

  1. Hongera timu ya Top Land, najua mmewaonea ndugu zetu wa Mpo Africa, mwakani mjiandae kukutana na Kurasini City ya Temeke

    JibuFuta