Open top menu
Jumanne, 3 Septemba 2013


Wakati pazia la usajili barani Ulaya limefungwa jana saa saba usiku kila timu ilikuwa ikihaha kuwania saini za wachezaji wanaowataka katika msimu huu.

Katika mbio hizo timu ya Manchester United ambayo imekuwa ikihaha kuimarisha katika nafasi yake ya kiungo, imefanikiwa kumnasa kiungo wa Everton, Marouane Fellaini dakika za mwisho kabla ya usajili huo kufungwa.

Manchester United imefanikiwa kumnasa Mbelgiji huyo kwa ada ya uhamisho wa pauni 27.5 milioni (zaidi ya Sh 60 bilioni) na kmuungana na meneja wake wa zamani David Moyes.

Manchester United pia wamewakosa wachezaji Ander Herrera wa Athletic Bilbao, Sami Khedira na Fabio Coentrao wote wa Real Madrid.

Moyes alisema: "Nimefanya kazi ya Marouane kwa miaka mitano na nimefurahi kwa uamuzi wake aliochukua wa kujiunga na Manchester United. Kiungo huyu huwa anacheza kwa uwezo mkubwa na natumaini ataleta mabadiliko katika kikosi changu."

Pia Arsenal wamefanikiwa kumnasa kiungo mshambuliaji wa Real Madrid, Mezus Ozil kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi kwa klabu hiyo wa pauni 42.5 milioni (zaidi Sh 103 bilioni).

Muda mchache kabla ya usajili kufungwa klabu ya Everton waliwasaini wachezaji Romelu Lukaku akitokea Chelsea, James McCarthy wa Wigan na kiungo wa Manchester City, Gareth Barry.

West Brom nao wamefanikiwa kunasa saini za wachezaji Stephane Sessegnon na Victor Anichebe wakitokea katika klabu ya Sunderland, Wakati Cardiff City wamemsajili Peter Odemwingie na Fabio Borini wa Liverpool na Andrea Dossena wamejiunga Sunderland kwa mkopo.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments