Open top menu
Jumapili, 22 Septemba 2013


WACHEZAJI wa Azam FC kwa pamoja wameahidi ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya Yanga utakaochezwa kwenye uwanja wa taifa, Azam FC ikiwa nyumbani.

Ahadi hiyo ilitolewa na wachezaji mbele ya viongozi wao (Makocha Kaly Ongala na Ibrahim Shikanda, Mwenye kiti Said Muhammad, Katibu Mkuu Nassor Idrissa na Mratibu wa timu hiyo Patrick Kahemele) kwenye kikao cha pamoja kati ya wachezaji na viongozi kutathmini mwenendo wa timu hiyo baada ya mechi nne za mwanzo za ligi kuu.

Wachezaji wa Azam FC wakiongozwa na John Bocco, Jabir Aziz na Salum Abubakar, walisema matokeo ya sare nyingi walizopata katika mechi zilizopita hayatokani na matatizo ya huduma isipokuwa ni mitihani ya kawaida kwenye soka ambapo timu inaweza kucheza vizuri nab ado ikashindwa kupata matokeo. Wachezaji wameahidi kuongeza nguvu kwa kuanzia mechi ya leo ili kupata matokeo ya ushindi badala ya sare.

Wachezaji kwa pamoja walionesha masikitiko yao kwa matokeo yaliyopita na kuahidi kuongeza kujituma kwenye mazoezi na mechi ili kurudisha makali yaliyoifanya Azam FC kuwa timu ya kuogopwa.

Azam FC itashuka uwanjani leo kukwaana na Yanga SC ambapo katika mechi nne zilizopita Azam FC imeambulia kipigo toka kwa Yanga. Lakini timu zote mbili zinashuka uwanjani zikiwa na matokeo ya kufanana na idadi sawa ya pointi baada ya kucheza michezo minne kila moja, kusinda mmoja na kutoka sare michezo mitatu hivyo kuwa na pointi sita.

Azam FC leo itamkosa Agrey Morris Ambrose ambaye alipewa kadi nyekundu kwenye mechi iliyopita dhidi ya Ashanti United na nafasi yake itajazwa na David Mwantika.

Kikosi kinachoanza leo ni

AISHI SALUM
ERASTO NYONI
WAZIRI SALUM
JOCKINS ATUDDO
DAVID MWANTIKA
HIMID MAO
KIPRE BOLOU
HUMPHREY MIENO
JOHN BOCCO
BRIAN UMONY
FARID MUSSA MALIK
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments