Open top menu
Jumanne, 17 Septemba 2013


 KIPUTE cha Ligi ya Mabingwa Ulaya kinaanza leo katika viwanja nane ambapo miamba 16 itavaana kuwania ushindi katika michezo hiyo ya raundi ya kwanza ya michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.

Katika michezo hiyo nane, macho ya mashabiki wa soka duniani kote yatakuwa katika michezo kati ya Manchester United ya England na Bayer Leverkusen ya Ujerumani mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Machezo mwingine ambao utavuta hisia za mashabiki wa soka ni ule utakaozikutanisha timu za Galatasaray ya Uturuki ambayo itawakaribisha Real Madrid kwenye Uwanja wa Turk Telekom Arena.
     
Mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Bayern Munich  watashuka uwanjani kuanza kutetea taji lao dhidi ya CSKA Moscow mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Allianz Arena.

Olympiacos watawakaribisha Paris Saint German ‘PSG’ mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Karaiskakis wakati Benfica nao watakuwa nyumbani kuwakabili Anderlecht          kwenye Uwanja wa Estadio da Luz.

Mchezo mwingine utakuwa kati ya Real Sociedad  na Shakhtar Donetsk huu utapigwa kwenye Uwanja wa Anoeta  na FC Copenhagen watavaana na Juventus kwenye Uwanja wa Parken.

Manchester City wao wataanza kampeni za Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Plzen mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Struncovy Sady. Michezo yote itaanza saa 3: 45 Usiku.

Michuano hiyo itaendelea tena kesho kwa michezo nane ambapo ratiba yake itakuwa hivi

FK Austria Vienna      v       FC Porto                       Franz Horr         
Atletico Madrid           v       Zenit St Petersburg      Vicente Calderon
Barcelona           v       Ajax                              Camp Nou         
Marseille                       v       Arsenal                         Stade Velodrome
AC Milan                    v         Celtic                            San Siro             
Napoli                           v       Borussia Dortmund     San Paolo           
Schalke 04                    v       Steaua Bucuresti          Veltins Arena    
Chelsea                         v       Basle                             Stamford Bridge
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments