Open top menu
Jumatano, 4 Septemba 2013


Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameonyesha kusikitishwa kwake kwa kuuzwa kwa mchezaji mwenzake, Mesut Ozil kwa klabu ya Arsenal huku akionyesha nia ya kuongeza mkataba mpya wa kuitumikia klabu hiyo.

Ronaldo ambaye amekuwa akihusishwa mara kwa mara kutaka kurudiu katika klabu yake ya Manchester United amefunguka na kusema kuwa anatarajia kuongeza mkataba mpya wa kuichezea timu hiyo kabla ya wasasa haujamalizika.

Staa huyo wa Ureno amebakisha miaka miwili kabla ya mkataba wake kumalizika lakini amesema kuwa atasaini mkataba mpya siku za hivi karibuni akiwa ni mtu mwenye furaha kuendelea kubaki Santiago Bernabeu.

Akimzungumzia Ozil, Ronaldo alisema amepokea kwa masikitiko taarifa za kuuzwa mchezaji huyo kwani alikuwa ni mtu anayejua nyendo zake za kufunga, “Ozil alikuwa msaada wangu mkubwa sana katika kufunga mabao.”

Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments