Open top menu
Ijumaa, 6 Septemba 2013


Uongozi wa klabu ya Yanga umewapiga chenga ya mwili wazee wa klabu hiyo baada ya kukanusha kufanyika kwa mabadiliko yaliyofanyika kuondolewa kwa katibu wake, Lawrence Mwalusako na nafasi yake kuchukuliwa na Mkenya.

Wazee wa Yanga walitoa tamko lao juzi kuupa uongozi huo masaa 24 kumtimua kati huyo mpya, Patrick Naggi hali iliyosababisha uongozi huo kukutana na kujadili suala hilo.

Akizungumza Nyumba ya Michezo na  Burudani, Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Clement Sanga alisema taarifa za kuondolewa Mwalusako na kuajiriwa Mkenya hazina ukweli kwamba tayari kuna mtu amechukua nafasi yake, kilichotokea ni kutokuwepo kwa mawasiliano mazuri katika suala hilo kati ya viongozi na wazee.

Sanga alisema kilichopo ni kwamba uongozi wa klabu ya Yanga upo katika mchakato wa kuhakikisha unajaza nafasi zilizopo wazi za mkurugenzi wa ufundi, mkurugenzi wa masoko, mkurugenzi wa fedha na zoezi hilo linaendeshwa na kampuni moja ambayo waliipa nafasi ya kuendesha zoezi hilo.

Zoezi likiwa ndani ya mchakato mmoja wa waombaji wa nafasi hizo Patrick Naggi aliwasili makao makuu ya klabu ya Yanga kwa lengo la kutaka kujua mazingira ya ufanyaji kazi yakoje na kufahamu baadhi ya mambo kuhusiana na klabu ndipo kulipotokea kutokuelewana na baadi ya wanachama wakiwemo wazee waliokuwepo eneo la klabu.

Makamu huyo alisema anapenda kutoa taarifa kwa umma na wanachama wa Yanga kuwa uongozi bado haujatoa baraka za ajira kwa mtu yoyote katika nafasi hizo, isipokuwa ni muombaji aliwahi kufika makao makuu kabla ya mchakatao wa usahili kukamilika.

Alisema Mwalusako anaendelea kuwa kaimu katibu mkuu wa Yanga mpaka hapo kutakapokuwa na taarifa nyingine zozote za mabadiliko kwa nafasi zote zilizopo wazi katika idara mbalimbali.

Uongozi unawaaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa soka kuwa kitu kimoja katika kuunga mkono harakati za kimaendeleo ili kuifanya timu iende katika hatua nyingine ya ushindani wa kimatifa.


Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments