Open top menu
Jumapili, 15 Septemba 2013


PAMOJA na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Abdallah Kibadeni amefunguka na kusema kuwa timu yake haipo vizuri.

Kibadeni ambaye ameanza kukinoa kikosi cha Simba msimu huu na tayari ameshacheza mechi tatu za mashindano na kufanikiwa kushinda michezo miwili na kutoka sare mechi moja.

Simba ilifungua pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kucheza na Rhino Rangers ya Tabora na kuvuna pointi moja baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na walikusanya pointi tatu dhidi ya JKT Oljoro kwa kushinda bao1-0, hivyo matokeo ya jana yanawafanya wafikishe pointi saba. 
Akizungumza na Nyumba ya Michezo na Burudani, Kibadeni alisema pamoja na kupata matokeo hayo lakini kikosi chake bado hakijakamilika kama vile anavyotaka yeye.

“Nikiwa kama kocha kuna aina ya uchezaji ambao nautaka timu yake icheze lakini bado,” alisema Kibadeni. “Siwezi kuridhika na ushindi ninaoupata. Kuna mambo yanataka wachezaji wangu wafanye.

“Kikosi changu bado hakijawa kamili kama ninavyotaka na mambo hayo yakitimia Simba itakuwa tishio zaidi ya hivi inavyoonekana sasa. Tukishacheza michezo mitano nadhani tutakuwa vizuri zaidi.”
Mchezo wa nne wa mashindano wa Kibadeni akiwa na Simba utachezwa Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa watakapovaana na Maafande wa Mgambo Shooting wakati mchezo wa tano utakuwa dhidi ya Mbeya City katika uwanja huo huo.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments