Open top menu
Jumatatu, 16 Septemba 2013


KIUNGO wa klabu ya Yanga, Mnyarwanda Haruna Niyonzima amefichua siri iliyomsababisha akachelewa kujiunga na timu yake iliyokuwa jijini Mbeya hivyo kukosa mchezo wao dhidi ya Mbeya City uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Niyonzima ambaye ndiyo roho ya Yanga kwa sasa, aliukosa mchezo huo baada ya kujiunga na mwenzake siku ya mchezo huo huku akiwa mgonjwa hivyo Kocha wake, Ernie Brandts hakumtumia katika mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya mabao 1-1.

Akizungumza na Nyumba ya Michezo na Burudani, Niyonzima alisema kuwa kilichomsababisha kuchelewa kurudi ni matatizo ya mgongo aliyoyapata alipokuwa akiitumikia timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’ katika mchezo wake wa kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia mwakani.

Niyonzima alisema alipokuwa katika kambi ya timu ya Amavubi alishtua tatizo lake la mgongo ambalo linamsumbua kwa muda mrefu hivyo alilazimika kubaki kwa ajili ya matibabu zaidi na alipomaliza ndipo alipoamua kurudi.

“Haikuwa busara kuwahi kurudi wakati bado naumwa. Sasa nimepona na nipo fiti kuitumikia klabu yangu ya Yanga kwa mafanikio zaidi,” alisema Niyonzima.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments