Open top menu
Jumatatu, 23 Septemba 2013


KLABU ya Sunderland imemtupia virago kocha wake, Paolo Di Canio kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo katika Ligi Kuu ya England.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imethibitisha kuwa Di Canio mwenye umri wa miaka 45, ametimuliwa kuinoa timu hiyo ikiwa ni masaa 24 baada ya kupoteza mchezo wake dhidi ya West Brom ambao walifungwa mabao 3-0.

Timu hiyo ambayo hadi sasa ipo mkiani katika msimamo wa ligi hiyo kupitia taarifa yake ilieleza: "Sunderland AFC imethibitisha kuwa imesitisha mkataba wa kocha wake mkuu Paolo Di Canio jioni hii."

Nahodha wa zamani wa Sunderland, Kevin Ball ameteuliwa kuiongoza klabu hiyo hadi hapo atakapopatikana kocha wa kudumu na ataanza kibarua hiyo kesho katika mchezo wa Kombe la Capital One dhidi ya Peterborough United.

Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments