Open top menu
Jumapili, 22 Septemba 2013


MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Mbeya City iliyochezwa jana (Septemba 21 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 123,971,000.

Watazamaji 21,936 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 32 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2.

Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 30,064,741.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 18,910,830.51.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 15,287,156.92, tiketi sh. 3,145,790, gharama za mechi sh. 9,172,294.15, Kamati ya Ligi sh. 9,172,294.15, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 4,586,147.08 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 3,567,003.28.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments