Open top menu
Ijumaa, 20 Septemba 2013


BINGWA ya dunia wa mita 200, Mjamaica Usain Bolt amesisitiza kuwa anatendelea kukimbia mbio za umbali huo katika michuano ya Jumuiya ya Madola mwakani.

Bolt ambaye ni bingwa mara sita wa Olimpiki anatarajia kushiriki michuano hiyo itakayofanyika mwakani katika mji wa Glasgow, lakini ataatoa uamuzi baada ya kujadiliana na Kocha wake, Glen Mills.

"Mbio hizo zipo katika mipango yangu," alisema Bolt, 27. "Natamani sana kushiriki lakini siwezi kwenda kinyume na kocha."

Mjamaica huyo alisema pamoja na kuzimudu mbio za mita 100 na 200 aliongeza: "Najisikia vizuri kukimbia mita 200, kama nikienda nitafanya hivyo kwa kuwa hizo ndiyo chaguo langu."

Bolt hajawahi kutwaa medali ya dhahabu ya michuano ya Jumuiya za Madola lakini alisema: "Tunaenda kujadiliana na kocha wangu, hatuna uhakika zaidi kama tutaenda kujadili na kuona kama kuna umuhimu wa kushiriki."
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments