Open top menu
Jumatatu, 2 Septemba 2013


 Kiungo wa pembeni Gareth Bale akikabidhiwa jezi namba 11 na Rais wa Real Madrid, Florentino Perez
Klabu ya Real Madrid imevunja mzizi wa fitina baada ya jana kumalizana na kiungo mshambuliaji, Gareth Bale kutoka Tottenham Hotspur kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi ya pauni 100 milioni.

Mchezaji huyo raia wa Wales amevunja rekodi ya mchezaji mwenzake wa timu hiyo,  Cristiano Ronaldo a mbaye alisajiliwa kwa ada ya uhamisho ya pauni 80 milioni mwaka 2009, hivyo kufanya timu hiyo kuwa na wachezaji waliosajiliwa kwa gharama kubwa.

“Napenda kuwashukuru kila mtu katika klabu yangu, Mwenyekiti,  bodi, wafanyakazi wote, kocha na wachezaji wenzangu na zaidi mashabiki ambao naamini watanielewa kwa maamuzi ytangu ya ajabu ya kumaliza maisha yangu katika klabu yangu," alisema Bale alipokuwa anazungumza na tovuti ya Tottenham.

“Nina uhakika kuwa huu ni wakati mzuri kuondoka katika ambayo nilikaa vizuri na kucheza soka zuri katika siku zote zilizokuwa pale. Najua wachezaji wengi wanapenda kujiunga na klabu bora yenye wachezaji wenye vipaji, lakini ninachoweza kusema, ndoto yangu imetimia.

“Pamoja na kuondoka lakini Tottenham ipo moyoni mwangu wakati wowote na nina uhakika msimu huu utakuwa wa mafanikio kwao. Sasa naangalia mbele, kinachofuata katika maisha yangu ni kucheza soka katika klabu ya Real Madrid.”

Wakati Madrid wakikamilisha kumnunua Bale wamemruhusu kiungo wake, Kaka kutua katika klabu ya AC Milan ya Italia. Madrid walikubaliana na Milan lakini walikuwa wakisubiri kukamilisha usajili wa Bale.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments