Open top menu
Ijumaa, 20 Septemba 2013


BEKI wa kulia wa Simba, Nassor Said ‘Chollo’ ataukosa mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Nahodha huyo wa Simba hakuwa uwanjani katika mchezo wao dhidi ya Mgambo Shooting kutokana na kuwa majeruhi baada ya kuumia nyonga katika mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar.

Akizungumza na Nyumba ya Michezo na Burudani, Chollo alisema hataweza kucheza mchezo wao unaofuata dhidi ya Mbeya City kwani daktari wa timu hiyo amemtaka kuwa nje kwa wiki mbili.

Chollo alisema pamoja na kuwa nje lakini hana wasiwasi wa kikosi chake kwani anaamini kuwa watafanya vizuri na wataendeleza wimbi la ushindi ulioanza na klabu yake na kuendelea kubaki kileleni.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments