Open top menu
Jumamosi, 14 Septemba 2013

Kiungo mshambuliaji wa Chelsea, Juan Mata




KIUNGO wa Chelsea, Juan Mata amesisitiza kwamba hana wasiwasi kugombania namba katika kikosi hicho na kwamba ataendelea kuitumikia timu hiyo.

Willian amekuwa kiungo mpya mshambuliaji katika kikosi cha kocha Jose Mourinho baada ya kusajiliwa kwa Andre Schurrle na kurudi kwa Kevin de Bruyne aliyekuwa kwa mkopo Werder Bremen.

Victor Moses amejiunga kwa mkopo wa muda mrefu Liverpool lakini Oscar naEden Hazard wameendelea kuwa wachezaji muhimu katika kikosi hicho cha Stamford Bridge, na Mata amekuwa si mchezaji wa kikosi cha kwanza tangu kuanza kwa msimu huu kutokana na kuwa majeruhi.

Lakini  yupo vizuri na anafanya mazoezi lakini amekumbana na wimbi la wachezaji wengi vijana wenye vipaji kitu kinachofanya apate ushindani kutokana na wachezaji hao.

"Nia yangu haijabadilika.Nitakuwa mzuri kama nilivyokuwa katika misimu mwili iliyopita na ikiwezekana nizidi zaidi kuwa mchezaji bora."

Kiungo wa Hispania aliiambia Sky Sports kwamba: "Ninafikiri ni vizuri kwa klabu, kwa kikosi na kwa meneja.

"Ninafikiri ni wazuri - De Bruyne, Schurrle, Willian, ni wachezaji wadogo na ni bora.Kila mmoja ana nafasi yake, ana ufundi wake na ninachoamini wote hao watatupa makubwa na ni vizuri tukawa na kikosi cha ushindani.

"Ningetarajia tungecheza wote sita lakini haiwezekani.Lakini ni vizuri kwa klabu katika mashindano yote tutakayoshiriki msimu huu."

Aliulizwa kwamba anaweza kucheza kama ilivyokuwa awali mara kwa mara, Mata alijibu: "Nina uhakika kwa hilo.Niwe muwazi imekuwa ngumu tangu niwe majeruhi, hivyo ninafanya mazoezi kidogo na wenzangu lakini sasa ninajisikia vizuri na ninaangalia mbele zaidi kucheza.

"Nitafanya kila niwezalo niwe kama misimu miwili iliyopita na nitajaribu kufunga, kutengeneza na timu ishinde."

Alipoulizwa kwamba Mourinho atarajie nini kutoka kwake,Mata alisema: "Tulizungumza kuhusu hilo na akasema nina umuhimu kwake na katika kikosi, kwahiyo nia yangu ipo pale pale.Ninatakiwa kuwa mzuri kama nilivyokuwa."

Mata alihusishwa kuondoka timu hiyo wakati wa kipindi cha usajili kilichopita lakini alisema hakutilia maanani hizo tetesi na hakufikiria kuondoka.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments