Open top menu
Jumatatu, 23 Septemba 2013


Baadhi ya viongozi wapya wa Chama cha mchezo wa Ngumi Mkoa wa Dar es salaam (DABA) wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa uchaguzi huo, Zuwena Kipingu katikati pamoja na mwangalizi mkuu wa uchaguzi, Remmy Ngabo (kulia) mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi wao mwishoni mwa wiki iliyopita

SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) halitambui uongozi uliojiingiza  madarakani wa kuongoza  chama cha ngumi mkoa wa Dar es salaam (DABA ) kiujanja ujanja bila kuzingatia Sheria na Kanuni za Baraza la Michezo Tanzania (BMT), katiba ya Chama cha ngumi cha dunia  (AIBA), Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) na katiba ya Chama cha Ngumi mkoa wa Dar es salaam (DABA).

Uongozi huo ulijingiza madarakani tarehe 21/09/2013 katika ukumbi wa DDC Mlimani bila ya kuwa na kibali cha kutoka BFT wala kibali kutoka Ofisi ya afisa michezo wa mkoa wa Dar es Salaam, ambao wao kiutaratibu ndio walikuwa na mamlaka ya kutoa kibali cha kufanyika kwa uchaguzi huo na kuusimamia kwa mujibu wa sheria zinazoongoza michezo nchini.

Badala yake genge la watu wachache walijikusanya na kupeana fomu kinyume na taratibu kwa kujuana na hatimaye kupeana taarifa wakakutana na kujivika madaraka kwa nyadhifa mbalimbali bila kufuata taratibu.

BFT haikubaliani na jambo hilo kwa kuwa kati ya  waratibu wa zoezi hilo waliojivika uongozi wa juu ni wale waliokuwa katika uongozi wa shirikisho la ngumi Tanzania BFT na kupelekea Tanzania kufungiwa uanachama na chama cha ngumi cha dunia (AIBA) kwa miaka miwili.

Pia viongozi hao ni wale waliosababisha bondia aliyekuwa tegemeo na Taifa, Petro Mtagwa kufungwa jela miaka 15 nchini Mauritius pia kusababisha bondia Emillian Patrick kushindwa kushiriki Mashindano ya Olimpiki 2008 baada ya kuwa amefuzu kwa tuhuma za kula njama za kusafirisha madawa ya kulevya.

Kibaya zaidi wengi waliopewa madaraka hawakujaza fomu za kuomba nafasi kama walivyopewa na  hawakuwepo katika uchaguzi huo, wala hawakufanya usaili kama taratibu zilivyo.

Wanachama halali waliokuwa wanatakiwa kuwepo katika uchaguzi huo mfano viongozi wa chama cha ngumi Temeke hawakupewa taarifa za uchaguzi na wameleta malalamiko ofisi za BFT.

Uchaguzi huo umekiuka katiba kwa kuhusisha mabondia na viongozi wa ngumi za kulipwa kitu ambacho ni tofauti na katiba zote za ngumi za ridhaa.

BFT itachukua hatua kali za kimaadili na kinidhamu kwa wote waliohusika na zoezi hilo na kusisitiza kwa wanachama wote kuzingatia sheria za uchaguzi wanapofanya uchaguzi wa vyama vyao na kuwataka wengine kutokujiingiza kwa magenge ambayo historia inaonyesha wamekuwa wasubufu wa mambo mbalimbali tokea uongozi wa Narcis Tarimo enzi za TABA kwa maslahi yao binafsi.


Zaidi tutashirikiana na Ofisi ya Afisa michezo wa Mkoa kuhakikisha uchaguzi unafanyika wa kupata viongozi  kwa kuzingatia taratibu.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments