Open top menu
Ijumaa, 13 Septemba 2013


STAA wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Snura Mushi anatarajia kurudi nkwa kishindo katika movie hivi karibuni kwa kiachia filamu ya Majanga ya Snura ambayo inatokana na wimbo wake uliotikisa wa Majanga.

Snura ambaye kwa sasa anafanya vizuri katika muziki na kibao chake cha Nimevurugwa ameuambia mtandao wa Nyumba ya Michezo na Burudani  alisema kuwa movie hiyo inatarajiwa kuwa hewani kabla ya kumalizika kwa mwaka huu.

Msanii huyo ambaye anasifika kwa uhodari wake wa kuzungusha kiuno alisema kila wimbo wake ukianzia na Majanga utakuwa na movie yake na kwa kuanzia atatoa filamu ya Majanga mwishoni mwa mwaka huu ikifuatiwa na movie aliyoigiza katika nje nne zikiwemo Tanzania, Zambia, Zimbabwe na Afrika Kusini inayoitwa Mzamiaji.

“Mimi nitakuwa mhusika mkuu katika movie ya Majanga na filamu nyingine zote zitakapokuwa kwenye series za nyimbo zangu na kuwashirikisha mastaa watakaokuwemo kwenye video zangu na wengine watakuwa mastaa wachanga.

“Lengo kupitia filamu hizi niwainue wasanii wa filamu ambao ni wachanga ili wapate nafasi ya kuonekana. Mastaa watakuwa wale tu walioigiza video za nyimbo zangu pekee,” anasema Snura.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments