Open top menu
Jumamosi, 14 Septemba 2013



Kiungo wa mpya wa Manchester United, Marouane Fellaini



KIUNGO mpya wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza, timu ya Manchester United, Marouane Fellaini amesema anataka yale yaliyofanywa na nahodha, Roy Keane.

Fellaini alitarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kitakachocheza na Crystal Palace jana baada ya kukamilisha uhamisho wa paundi milioni 27.5 katika siku ya mwisho ya kufunga dirisha.

“Kocha wangu ndiye atakayejua sehemu gani ya kunichezesha ila ningependa zaidi niwe kiungo mkabaji”

"Keane alikuwa ni mchezaji wa kipekee ambaye alikuwa ana uwezo wa kucheza mipira yote.Labda ninaweza kufanya aliyofanya," alisema nyota huyo wa Ubelgiji, 25 aliyejiunga akitokea Everton.

"Ninaweza kuzuia mipira.Ninaweza kuokoa na ninaweza kucheza sehemu iliyo wazi."

Mchezaji wa zamani wa Ireland, Keane ambaye aliichezea United kuanzia 1993 mpaka 2005, alikuwa nguzo imara wakati wakitwaa vikombe saba vya michuano mbalimbali.

Kiungo huyo ambaye sasa ana miaka 42, pia alimsaidia Sir Alex Ferguson kutwaa Ligi ya Mabingwa mara moja, Kombe la FA mara 4 Ngao ya Hisani mara 4 na ubingwa wa mabara mara moja.


Mbali na hilo, Moyes pia alisema ataangalia jinsi gani atakavyoweza kuangalia kumchezesha Wayne Rooney, kutokana na kuwa majeruhi.
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments