Open top menu
Jumatano, 18 Septemba 2013


JANA klabu ya Manchester United ilianza vizuri kampeni yake ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi mnono wa mabao 4-2 dhidi ya timu ya Bayer Leverkusen mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Mbali na ushindi huo lakini kupitia mchezo huo klabu hiyo imeweka rekodi tatu muhimu kwa wachezaji wake pamoja na kocha wao ambazo zimewafanya wahusika wake kulala usingizi mnono baada ya mchezo huo.

Rekodi ya kwanza iliyowekwa katika mchezo huo ni ya mshambuliaji wa klabu hiyo, Wayne Rooney ambaye jana alifunga mabao mawili katika ushindi huo na kumfanya aendelee kuwa mchezaji pekee wa England aliyefunga mabao mengi katika michuano hiyo.

Rooney anashikilia rekodi hiyo baada ya jana kutimiza mabao 29 akifuatiwa na mchezaji mwenzake, Paul Scholes aliyefunga mabao 24 wakati nafasi ya tatu inashikiliwa na Frank Lampard wa Chelsea aliyefunga mabao 22 na Steven Gerrard yupo nafasi ya nne baada kufunga mabao 19, nafasi ya tano inashikiliwa na Andy Cole aliyefunga mabao 18.

Mchezaji mwingine ambaye jana ilikuwan siku yake muhimu baada ya kumaliza mchezo huo ni kiungo mpya wa timu hiyo, Marouane Fellaini ambaye alicheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Manchester United

Fellaini hakuwahi kucheza mashindano hayo kwani tangu alipotua Everton 2008 klabu hiyo haikuwahi kupata nafasi ya kushiriki michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.
Mara baada ya mchezo huo Fellaini aliandika kwente ukurasa wake wa Twitter: “Hii ni siku yangu muhimu sana. Nimetimiza ndoto yangu ya pili katika maisha ya soka.” Ndoto ya kwanza kucheza katika klabu kubwa kama Manchester United.

Pia kocha wa klabu hiyo, David Moyes ameweka rekodi ya kurudi katika rekodi ya kukaa kwenye benchi wakati timu yake ikiwa inashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya miaka nane.

Mara ya mwisho alikaa kwenye benchi mwaka 2005 akiwa na Everton baada ya kumaliza msimu wa 2004/05 ikiwa nafasi ya nne katika Ligi Kuu ya England
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments