Open top menu
Ijumaa, 20 Septemba 2013


BINGWA wa tenisi wa Wimbledon, Andy Murray hataonekana kwenye uwanjani kwa msimu mzima uliobaki kutokana na kufanyiwa upasuaji wa mkono wake.

Murray mwenye umri wa miaka 26, ataikosa michuano ya Wazi ya Ufaransa kiutokana na majeruhi hayo aliyoyapata lakini anatarajiwa kurudi uwanjani mwanzoni wa msimu ujao wa michuano ya tenisi.

Mchezaji tenisi huyo mwenye rekodi ya kuwa Muingereza wa kwanza kutwaa taji la Wimbledon kwa miaka 77 iliyopita alitarajiwa kushiriki katika fainali za tenisi za London mwezi Novemba lakini sasa ndoto hiyo imetokewa na hataqweza kucheza michuano yote iliyobaki ya msimu huu.

Murray aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook: "Nashukuru kwa ujumbe mzuri niliopokea siku ya leo... Natarajiwa kufanyiwa upasuaji Jumatatu. Kila mtu atajua kila kinachoendelea. Nitarudi tena uwanjani nikiwa fiti zaidi."
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments