Open top menu
Ijumaa, 13 Septemba 2013


KUNDI la muziki wa kizazi kipya la East Coast Team ‘ECT’ lenye maskani yake Upanga Mashariki, ambalo hivi karibuni limerudi tena kwenye tasnia hiyo na tayari wameanza kutupa mawe kwa mahasimu wao wakubwa TMK Wanaume.

ECT ambalo lilipata umaarufu mkubwa mwanzoni mwa miaka ya 2000 lakini lilivunjika baada ya wasanii wake mahiri kuanza kufanya kazi zao binafsi wakati TMK Wanaume waligawanyika na kuzaliwa makundi mawili TKM Wanaume Halisi na TMK Wanaume Family.

Kundi la ECT linaloongozwa na Gwamaka Kaihula anayejulikana zaidi kama King Crazy GK limeundwa upya likiwa na wasanii walewale na wengine wapya na tayari wameanza kutambulisha ujio wao mpya kwa kuachia wimbo mpya wa kiongozi wa kundi hilo GK uliopewa jina la ‘Baraka au Laana kuzaliwa Afrika’.

Wasanii wanaounda kundi hilo kwa sasa ni GK, Ambwene Yessaya ‘AY’, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’, Adam Semkwiji ‘Snare’, Benjamin Gemba ‘Buff G’, Juma Mtanga, Sheila ‘Lady Slay’, Sharrif na Yussuph Seleman ‘Yuzo’ na wengine wanatarajia kuongezeka baada ya kufanyika mchujo wa wasanii wenye uwezo wa kuingia katika kundi hilo.

GK alipokuwa akizungumza na Nyumba ya Michezo ya Burudani alisema kwa sasa wamerudi kwa kishindo na wamekuja kivingine kabisa na kiukweli hawawezi kushindana na TMK Wanaume kwani kwa sasa hawawezi kuwaita washindani wao kwa kuwa hawawezi kufikia viwango vyao walivyokuja navyo sasa.

“Inakuwa ngumu kusema tumerudi kushindana na TMK kwani wakati wapo pamoja walikuwa hawatuwezi sasa wametengana ndiyo kabisa hawawezi kuufikia muziki wetu,” anasema GK. “Labda warudi waungane upya na wafanye muziki kwa viwango vya kimataifa ndipo wataweza kushindana na sisi.”

GK alisema anaomba kundi la TMK lirudi na wafanya muziki kwa kiwango chao ili waweze kuwa na ushindani kwani bila ushindani muziki hauwezi kuendelea lakini pia hamasa ya muziki utakuwa chini kwa kuwa hakuna kitu ambacho kinawafanya wasanii wafanye kazi kwa bidii.

GK alisema: “Enzi zile kulikuwa na watu wanatembea kwa miguu kutoka Temeke hadi Diamond kuja kuangalia show ya ECT na Wanaume. Show ambazo ECT na Wanaume walikuwepo zilikuwa zinafanya vizuri sana kutokana na ushindani wa makundi haya.”
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments