VINARA wa Ligi Kuu ya England, Arsenal wamejiweka
njia katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (Uefa) baada ya leo usiku
kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Borussia Dortmund.
Kwa matokeo hayo Arsenal wamejiweka katika mazingira
magumu kusonga mbele kwani wanakabiliwa na michezo migumu ambayo watakuwa
ugenini.
Matokeo ya mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa
Emirates, Arsenal ipo katika nafasi ya pili katika Kundi F, ikiwa na pointi
sita sawa na kminara wa kundi hiyo, Dortmund lakini pia ipo sambamba na Napoli
wanaoshika nafasi ya tatu katika kundi hilo wakiwa na tofauti ya mabao.
Arsenal ndiyo wanaonekana kuwa katika mazingira
magumu kutokana na kuwa na michezo miwili ya ugenini dhidi ya Napoli na
watakaporudiana na Dortmund kabla ya kumaliza na Marseille Emirates, ili waweze
kusonga mbele wanatakiwa kushinda michezo hiyo.
Dortmund ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao la
kuongoza katika mchezo huo kupitia kwa kiungo wake Henrikh Mkhitaryan dakika ya
16 lakini mshambuliaji wa Ufaransa, Olivier Giroud aliisawazishia Arsenal
dakika ya 41.
Mashabiki wa Arsenal hawawezi kumsahau Robert
Lewandowski kwani ndiye alilizamishwa jahazi la timu hiyo baada ya kukwamisha
msumali wa mwisho dakika ya 87 kwa shuti kali akiunganisha krosi ya Kevin
Grosskreutz.
Mabao mawili ya Fernando Torres yaliiwezesha timu
yake ya Chelsea kupata ushindi wa ugenini dhidi ya Schalke 04 wa mabao 3-0 na
kuwafanya kuongoza kundi E.
Torres alifungwa bao la kwanza akiunganisha kichwa
krosi ya Branislav Ivanovic dakika ya 15 kabla ya kuongeza la pili dakika ya 69
na Eden Hazard alishindiliwa msumali wa mwisho.
Katika mchezo mwingine wa Kundi H, FC Barcelona
walishindwa kutamba wakiwa ugenini baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi
ya AC Milan, wenyeji ndiyo walikuwa na kwanza kupata bao kupitia kwa Robinho wakati
bao la kusawazisha lilifungwa na Lionel Messi.
Matokeo mengine ya michezo ya leo ni kama ifuatavyo
Marseille 1 - 2 Napoli
Celtic
2 - 1 Ajax
Austria Wien 0
- 3 Atltico Madrid
Steaua 1 - 1 Basel
FC Porto 0 - 1 Zenit
0 comments