Mshambuliaji wa Yanga Hamis Kiiza akifunga bao la pili katika mchezo huo huku Haruna Shamte na kipa Abel Dhaira wakiwa wameduwaa
SIMBA imeonyesha kuwa bado ni wababe katika Ligi Kuu
ya Tanzania Bara baada ya kulazimisha sare wakiwa nyuma ya mabao 3-0 dhidi ya
wapinzani wao Yanga katika mchezo wa ligi hiyo uliochezwa leo kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo ambao ulihudhuriwa na mashabiki
lukuki kiasi cha kuuzaja uwanja huo, Simba walijikuta wakienda vyumbani wakiwa
tayari wamekubali kipigo cha mabao matatu huku wakiwaaacha Yanga wakitawala
mchezo kwa kipindi chote cha kwanza.
Yanga ambao walianza mchezo huo kwa kasi walipata
mabao yao kupitia kwa Mrisho Ngassa ambaye alitangaza kuchoma nyumba zake tano
kama hatafunga bao katika mchezo huo au kutoa pasi ya bao, hivyo kwa bao hilo
ameokoa nyumba zake.
Mabao mengine mawili ya Yanga yalifungwa na Mganda,
Hamis Kiiza akimalizia kazi nzuri za Didier Kavumbagu ambaye alimtengenezea
mabao yote mawili.
Mashabiki wa Yanga walijua tayari wamemaliza kazi
kwaki timu yao ilikuwa ikicheza soka safi huku wakiwa mbele kwa mabao matatu,
lakini kibao kiligeuka na wapinzani wao kurudi kwa kutawala kipindi cha pili na
kusawazisha mabo yote mawili.
Beki wa Simba, Joseph Owino akiwa makini kuhakikisha Mrisho Ngassa asilete madhara langoni mwao
Mabao ya Simba katika mchezo huo yalifungwa na
Betrum Mombeki, Said Hamis kabla ya Gilbert Kaze kuwaahamsha mashabiki wa Simba
ambao waliamini kuwa wamelala katika mchezo huo.
Simba: Abel Dhaira, Said Nassor, Haruna Shamte,
Gilbert Kaze, Joseph Owino, Jonas Mkude, Ramadhani Singano, Abdulhalim Humud/Said
Hamis, Betrum Mombeki, Amis Tambwe na Haruna Chanongo/Willium Lucian.
Yanga: Ali Mustafa, Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir
Haroub, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Haruna Niyonzima, Frank Domayo, Didier
Kavumbagu, Mrisho Ngassa na Hamis Kiiza/ Simon Msuva
0 comments