Kikosi cha Yanga
Kikosi cha Simba
MAGARI yenye shughuli maalumu tu ndiyo
yatakayoruhusiwa kuingia uwanja wakati wa mechi ya Simba na Yanga itakayochezwa
keshokutwa (Jumapili) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi itaanza saa 10 kamili jioni, na kila timu
inaruhusiwa kuingia na magari matatu tu; gari la timu na mengine mawili ya
viongozi. Ukaguzi wa kuingia uwanjani ni kwa watu wote, kwani utaratibu huo si
wa kumdhalilisha mtu bali lengo lake ni kuhakikisha usalama.
Vilevile watu hawataruhusiwa kuingia uwanjani na
mifuko ya aina yoyote ikiwemo mabegi, isipokuwa kwa waandishi wa habari
wanaotumia mabegi hayo kwa ajili ya kubebea kamera zao. Pia hakuna
wafanyabishara watakaoruhusiwa kufanya biashara katika maeneo yanayozunguka
uwanja.
Kwa washabiki watakaokuwa katika mazingira ya kuwa
kero kwa wenzao wakiwemo walevi hawataruhusiwa kuingia uwanjani, pamoja na wale
wenye silaha kama bastola ambapo wakikamatwa wafikishwa polisi na baadaye
kufunguliwa mashtaka kortini.
Barabara ya Uwanja wa Taifa itafungwa kuanzia saa 2
asubuhi upande wa Chang’ombe, hivyo washabiki wanatakiwa kununua tiketi zao
mapema kesho (Jumamosi) ambapo zitaanza kuuzwa katika vituo mbalimbali kuanzia
saa 4 asubuhi.
Vituo hivyo ni mgahawa wa City Sports Lounge, Shule
ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa
Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala, Uwanja
wa Uhuru, mgahawa wa Brake Point uliopo Kijitonyama na BMM Salon iliyoko Sinza
Madukani.
0 comments