SERIKALI ya Zambia imetoa vibali vya kukamatwa kwa
wachezaji wake watatu waliokosa mechi ya kirafiki dhidi ya Brazil mjini Beijing
China. Hata hivyo Zambia ilishindwa na Brazil mabao mawili kwa nunge.
Klabu ya DRC TP Mazembe ilisisitiza kuwa wachezaji
hao Rainford Kalaba, Stoppila Sunzu na Nathan Sinkala walijeruhiwa na
kusababisha mgogoro kati ya shirikisho la soka la Zambia na serikali ya Zambia.
Baada ya wachezaji hao kufanyiwa ukaguzi mjini
Lusaka, shirikisho la soka la Zambia likasisitiza kuwa bado wanaweza kusafiri
kwenda China kwa mchuano huo, lakini klabu ya Mazembe ambako wachezaji hao
hucheza soka ya kulipwa ikawatakaza kurejea.
Hatua hiyo ilisababisha serikali ya Zambia kuingilia
kati kwa kuwapokonya wachezaji hao pasi zao za usafiri ili kuwazuia kwenda
kuchezea klabu yao mjini Lubumbashi.
Hata hivyo, wachezaji walifanikiwa kuvuka mpaka na
wanaaminika kuwa nchini DR Congo.
Shirikisho la soka la Zambia limeandikia barua
shirikisho la soka duniani Fifa, na kulalamika kuwa klabu ya Mazembe
haikuwaruhusu wachezaji hao kushirki majukumu yao ya kimataifa.
Zambia ilishindwa kwenye mechi hiyo ya kimataifa
mjini Beijing
Zambia ambao ni mabingwa wa kombe la taifa bingwa
Afrika walikuwa wanashirki mechi yao ya kwanza wakiongozwa na kocha wao mpya
Patrice Beaumelle, ambaye alichukua usukani siku nane zilizopita baada ya Herve
Renard kucha kazi.
0 comments